Jumatano 4 Juni 2025 - 17:08
Maendeleo, Usalama na Ustawi ni kwa Kuendeleza Njia ya kiakili ya Imam Khomeini (ra)

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, asubuhi ya leo, mbele ya umati mkubwa na wenye hamasa katika Haram takatifu ya Imam Khomeini (ra), akizungumza kuhusu athari dhahiri za Mapinduzi ya Kiislamu katika mabadiliko ya dunia ya leo, alisisitiza kuwa: Imam mkubwa aliyepita, kwa busara na akili iliyochipua kutokana na imani, alikusanya misingi ya kuendeleza harakati ya mapinduzi yenye nguvu na heshima ya taifa chini ya dhana ya msingi ya "uhuru wa kitaifa", na Iran tukufu kwa msaada wa misingi hiyo, itafikia maendeleo, ustawi wa kijumla, usalama wa kudumu, kuinuka zaidi kwa nafasi yake kimataifa, na mustakabali wenye nuru.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei katika kufafanua suala la kitaifa la nyuklia, alilisema Iran kupata mzunguko kamili na wa kujivunia wa nishati ya nyuklia, ni matokeo ya imani ya taifa na wanasayansi vijana katika kaulimbiu ya "Sisi tunaweza". Akiashiria athari muhimu za sekta hii katika maendeleo ya sayansi na viwanda vingine, alilitaja pendekezo la nyuklia la Marekani kuwa linapingana kikamilifu na msingi huu wa kufungua njia wa "Sisi tunaweza", na akasisitiza kiwa: "Sekta kubwa ya nyuklia bila shughuli ya kurutubisha nyuklia haina maana yoyote," na Marekani na utawala wa Kizayuni wajue kwamba katika kutimiza lengo lao kuu la kuiangamiza sekta ya nyuklia ya Iran, hawataweza kufanya chochote.

Yeye (Kiongozi Mkuu) alimuelezea Imam Khomeini kuwa ni mbunifu mkuu wa mfumo thabiti, unaoendelea na wenye nguvu wa Jamhuri ya Kiislamu, na akasema: Miaka 36 baada ya kufariki mtu huyo mkuu, uwepo wake na athari za Mapinduzi yake zinaonekana katika mambo kama vile kuporomoka kwa madola makuu, kutokea kwa mfumo wa dunia wa matawi mengi, kushuka pakubwa kwa hadhi na ushawishi wa Marekani, kuongezeka kwa chuki dhidi ya uzayuni hata huko Ulaya na Marekani, na mwamko wa mataifa mengi na kukataa thamani za wamagharibi.

Kiongozi wa Mapinduzi, akielezea mshangao wa dunia ya Magharibi mbele ya “Basiji wa taifa la Iran wakiongozwa na mwanazuoni wa dini, ushindi wa Imam na taifa huku wakiwa mikono mitupu dhidi ya utawala wa Pahlavi uliokuwa umejizatiti kwa silaha, na uwepo wa Wamarekani na Wazayuni waporaji kutoka Iran”, alisema: "Mshangao wa pili wa Magharibi ulikuwa ni kuundwa kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa busara na juhudi za Imam."

Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Kiongozi wa Mapinduzi alimwita Marekani mshirika wa jinai za utawala wa Kizayuni, na akaongeza kwa kusema: "Ni kwa sababu hii ndio maana tunasisitiza kwamba Marekani lazima iondoke katika eneo hili."

Ayatollah Khamenei pia alitaja jukumu la serikali za Kiislamu kuwa ni zito, na akisisitiza kwamba "leo si wakati wa kujizuia, kuwa wa tahadhari, kutoegemea upande wowote au kunyamaza kimya," akaongeza kwa kusema: Iwapo serikali ya Kiislamu, kwa namna yoyote au kwa kisingizio chochote, iwe kwa kurekebisha mahusiano, au kwa kufunga njia za kuwasaidia watu wa Palestina, au kwa kuhalalisha jinai za Wazayuni, itaunga mkono utawala huo, basi hakika ijue kuwa fedheha ya milele itaandikwa kwenye paji la uso wake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha